Mh..Michael M.Ngayalina Mkuu wa wilaya Buhigwe amesikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi wa kata ya Nyamugali katika ziara yake ya kata kwa kata. Hata hivyo Ameagiza Eneo la ekari 7 lililouzwa na wajumbe wachache wa serikali ya kijiji bila idhini ya mkutano mkuu wa wananchi kurudishwa umiliki wa serikali ya kijiji na aliyenunua arudishiwe pesa
Hata hivo hakuwa mbali na wakuu wa taasisi mbalimbali na wakuu wa idara na vitengo katika kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi katika hilo
Aidha Amesisitiza Wazazi kuwapa mahitaji muhimu watoto wao ikiwa ni wajibu wa mzazi kumpatia mtoto wake haki zote ikiwemo kumunulia Uniform,Madaftari,viatu ili wasome Kwa bidiii
Wananchi wa kata hiyo wamempongeza mkuu wa wilaya Kwa ziara yake ya Kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo mbalimbali. Sio hivyo tu Wananchi wamefanya sala/Dua maaalumu ya kuombea serikali ya Awamu ya sita inayongozwa na MH Dr.Samia S.Hassan. mama shupavu kweli kweli.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz