Wakazi Wilayani Buhigwe leo Juni 1,2024 wamejitokaza katika zoezi la kufanya usafi kwenye mazingira yanayoizunguka Halmashauri hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo huadhimishwa Juni 1 Kila mwaka.
Usafi huo ulofanyika umejumuisha makundi mbali mbali kama ifuatavyo Ofisi ya Mkuu wa wilaya Buhigwe, Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Buhigwe, Taasisi mbali mbali zilipo Buhigwe na wananchi wa wilaya ya Buhigwe.
Ngayalina amewataka wananchi na watumishi wa wilaya ya Buhigwe kuweka mazingira Yao safi kwa kufanya usafi na iwe ni Desturi ya Kila mmoja katika maeneo Kila iitwapo Leo ili kuhakikisha tunatokomeza madharia ya mbu na Magonjwa yanayoambukizwa kwa uchafu Kauli mbiu ya mwaka huu ni Urejeshwaji wa Ardhi Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na ukame.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya amewapongeza watu wote kwa makundi yote kwa kujitokeza katika zoezi hilo kwa kusema kuwa waendelee na Ushirikiano huo,Umoja huo,Mshikamano huo, Upendo huo siku zote ili kuhakikisha Buhigwe yetu inang'ara.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz