Mhe. Kanali Michael Masala Ngayalina, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe amekabidhi leo jumla ya pikipiki 5 zenye dhamani ya Tsh 12,500,000 kwa vijana wajasiriamali wa kikundi cha Tuyajenge kinachofanya shughuli zake kwenye Kata ya Buhigwe Wilayani Buhigwe.
Kabla ya shughuli ya kuwakabidhi pikipiki hizo alipokea Taarifa kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Wilayani humo, Ndg. Christopher Kajange ambaye alieleza kuwa Halmashauri hiyo ilitenga Jumla ya Tsh 64,858,000 kwa ajili ya Vikundi vya Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 ambazo zote zimekwishakutolewa.
Katika taarifa hiyo ilieleza kuwa kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 Jumla ya Kiasi cha Tsh. 111,850,000 zimekopeshwa kwenye Vikundi 18 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu wilayani humo.
Baada ya kupokea taarifa hiyo DC Ngayalina alimpongeza Ndg. Essau Hosiana Ngoloka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na menejimenti yake kwa kusimamia kikamilifu utoaji wa mikopo hiyo na kuwafikia walengwa na kwa wakati:
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz