Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mh Kanali Isaac Mwakisu ambae ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amewataka wajumbe Wakuu wa kampeni ya Uandikishaji wa Vyandarua ngazi ya kaya kufuatilia kwa makini kuhakikisha vyandarua vinatumika kwa lengo lililokusudiwa.
Ameyasema hayo leo tarehe 22 mwezi Mei 2025 wakati wa Kikao cha utambulisho wa mdau wa kusafirisha vyandarua ambae ni bohari ya dawa(MSD) skilichofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe.
Kwa upande wake Peter Gitanya kutoka Wizara ya afya chini ya mpango wa taifa wa kudhibiti Maralia ameipongeza Wilaya ya Buhigwe kwa kufikisha asilimia 98 ya uandikishaji na kuwaasa kuongeza juhudi ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Naye Nyahiri Matinyi kutoka bohari ya dawa kanda ya Magharibi (MSD)amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hilo la usafirishaji wa vyandarua unafanyika kwa wakati na kwa muda mchache.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz