Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameyataka Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika Wilaya ya Buhigwe kuhakikisha inaleta mabadiliko ya maisha kwa Wananchi .
Ameyazungumza hayo leo tarehe 27 mwezi Juni 2025 katika jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya kiserikali lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Akizungumza amesema kuwa ni ajabu kuona mashirika hayo yatakuwa na miradi mbalimbali katika Wilaya ya Buhigwe lakini kutokuwa na mabadiliko yoyote yanayotokea katika maisha ya watu .
“Mimi napenda stori ambazo utaniambia kijiji Fulani nimefanya hiki na watu wenyewe hawa hapa ,sisi tunataka mabadiliko katika maisha ya watu na si mawasilisho mengi yasiyokuwa na faida kwa Wananchi”alisema Kanali Ngayalina.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi ameyataka Mashirika hayo kuhakikisha wanafaya kazi kwa ushirikiano na Halmashauri.
Akisoma taarifa Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Buhigwe Maria Minja amesema kuwa Halmashauri ina Jumla Mashirika yasiyo ya kiserikali 20 yanayo fanya kazi katika sekta za Elimu, Kilimo, Afya, Mazingira, Utoaji wa elimu ya Mapambano dhidi ya Ukatili na UKIMWI, Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz