Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina amewataka wanufaika wa mikopo kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya kuwainua kiuchumi.
Hayo yamejiri katika hafla ya kukabidhi mkopo wa Asilimia 10 wa zaidi ya sh.Milioni 100 kwa vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu halmashauri ya wilaya ya Buhigwe.
Ameongezea kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Rais Samia Suluhu Hassani na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo zinazotokana na mapato ya ndani.
Naye Mkururugenzi Mtendaji amewapongeza wote waliofanikiwa kupata fedha na kuwasihi kutumia fedha hizo kwa weledi ili kuunga mkono lengo la mh Rais la kukuza uchumi wa Wananchi na taifa.
Sambamba na hilo amewakaribisha wale wote wenye sifa za kupata mkopo huo kujitokeza kwa wingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Bw.Christopher Kajange amesema wataendelea kukopesha fedha kwa vikundi vya wajasiriamali lengo ikiwa ni kukuza uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz