Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mhe. Col. Michael Masala Ngayalina ameshiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kimara katika kata ya Kinazi wilayani humu na kuwapongeza wananchi kwa kuamua kujenga zahanati kwa nguvu zao wenyewe. Hayo yamefanyika mapema leo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, ambapo aliambatana na timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Buhigwe.
Akizungumza na wanachi wa Kata hiyo amesema" Maendeleo hayana chama hivyo nawaagiza kufanya kazi kwa ushirikiano kukamilisha ujenzi wa zahanati hii kwa wakati ilihuduma za matibabu zianze kutolewa kwa wananchi, yoyote atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria".
Aidha akijibu risala iliyosomwa na Mtendaji wa kijiji Bi Paula Mbehoma, Mhe Mkuu wa Wilaya akishirikiana na timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wametoa shilingi 1,500,000/= ikiwa ni kuwaongezea nguvu wanachi hao, pia ameahidi kwamba yuko tayari yeye na timu yake kutoa mchango wa hali na mali kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndg. Anosta L. Nyamoga amewapongeza watendaji wa vijiji vyote viwili vilivyoko kwenye kata hiyo pamoja na viongozi wengine kwa jitihada zao na weledi katika utendaji wa kazi.
Mwisho Mganga Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Dkt. Julius Nyasongo amesema eneo inapojengwa zahanati ni kubwa na linatosha kujengwa kituo cha Afya au Hospitali, hivyo nawaombeni wananchi msifikirie zahanati bali kituo cha afya au hospitali.
Hitimisho lilikuwa kwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Buhigwe Mhe. Albert Ntabaliba Obama ambapo alisema Ofisi yake inatoa mchango wa bundle 5 za bati kwa ajili ya kuezeka zahanati hiyo, naye Diwani wa kata ya Kinazi Mhe. Yusufu D. Degede ametoa shilingi 50,000/=.
Zahanati ya Kimara itahudumia vijiji vinne ambavyo ni Kinazi, Kimara, Mpungwe, na Nyanzozi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz