Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewataka Wananchi Wilaya ya Buhigwe kutumia fursa vizuri ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa inayotoka Uvinza mpaka Musongati Burundi kupitia vijiji vya Katundu na Kilelema kujinufaisha kiuchumi.
Ameyasema hayo katika mkutano alioufanya na Wananchi wa Kijijji cha Katund,Kilelema na maeneo ya jirani kikihusisha Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe,Wataalamu kutoka Shirika la reli Tanzania na Wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa reli hiyo.
Aidha ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa maendeleo mbalimbali katika Wilaya ya Buhigwe na Nchi kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa reli ya Kisasa itakayopunguza umbali wa kutoka Kigoma kwenda mikoa mingine kama Dodoma na Dar es salaam.
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo wa reli Mhandisi Mwita amesema kuwa mradi ni wa miaka sita hivyo Wananchi wa maeneo hayo na ya jirani kutumia fursa mbalimbali za ajira zitakazojitokeza ili kuwanufaisha wao kama Walengwa wa mradi huo.
Sambamba na hilo amewasihi Wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kutoa rushwa au kwa njia yoyote kwa madai ya kupewa ajira.
Mr Joh ni mkandarasi wa mradi huo,kwa upande wake amesema mradi huo utahusisha ajira kwa wazawa kwa asilimia 70 hivyo kuomba kupewa ushirikiano na Wananchi hao.
Sarah Chiza na Juma Kakozi wao ni Wananchi wa kijiji cha Katundu na Kilelema wamesema wamefurahia sana kuja kwa mradi huo wa ujenzi ambao unaenda kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji chao na Wilaya kwa ujumla na kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira kwa miaka sita.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amekabidhi mifuko 20 ya simenti aliyoahidi kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya Serikali ya Kijiji iliyojengwa kwa nguvu za Wananchi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz