Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mpendwa wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Kwa niaba ya watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe napenda kutoa pole kwa watanzania wote kufuatia msiba huu mkubwa wa kuondokewa na kiongozi wetu mkuu, mtetezi wa wanyonge, mpigania haki na mpenda maendeleo kwa taifa lake.
Niwaombe watanzania wenzangu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wetu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
Imetolewa na idara ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji mji wa Bwega
S.L.P 443, Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz