CHAMA Cha mapinduzi (CCM)Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kimeadhimisha maika 47 ya kuzaliwa kwa chama hicho huku kikijivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbali mbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayoonekana kwa macho.
Pia kimeridhishwa na namna Ilani ya uchaguziya CCM 2020_2025 ilivyotekelezwa na serikali kuwa imeutendea haki Mkoa wa Kigoma kwa miradi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo ya Kimkakati.
Kauli hiyo ilitolewa wilayani buhigwe na mwenyekiti wa CCM Wilaya Eng. Erneo Dyegula wakati akihutubia wananchi na wanachama wa chama hicho katika maadhimisho ya miaka 47 ya CCM Ngazi ya wilaya yaliyofanyika katika Kijiji Cha Nyakimue Kata ya Munanila tarafa ya Manyovu
Wakati maadhimisho hayo yakiendelea viongozi waliohudhuria walipata wasaa wa kusikiliza na kutatua kero mbali za wananchi walioshiriki maadhimisho hayo wilayani humo.
Akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa amesema kazi kubwa kwa wana Buhigwe ni kuongeza idadi ya wanachama wakizingatia mtaji wa biashara ni faida ili kuongeza kipato na mtaji wa siasa ni wanachama,hivyo wajisajili katika daftari la kudumu la wapiga kura,kujenga uwezo wa watendaji na wanawake wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.
Naye Katibu wa chama hicho wilaya ya Buhigwe, Salum Hajj amesema miaka 47 bado chama cha mapinduzi CCM kiko imara,kina mvuto na kitaendelea kuwa na mvuto kwa wananchi kutokana na kujipambanua kwa kazi nzuri zinazofanywa na kuleta maendeleo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz