Kufatia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mhe Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col Michael Masala Justine Ngayalina Azindua jengo la MAMA NGONJEA katika hospitali ya wilaya ya buhigwe ikiwa na moja ya jengo lenye tija kubwa kwa wanawake wajawazito kupata sehemu ya kupumzikia huku wakiwa chini ya uangalizi wa watoa huduma.
Amewataka wana buhigwe hususani wanawake ambao ni wajawazito na wanaoishi mbali na maeneo ya kutolea huduma za Afya kuwahi mapema au kabla ya muda wa kujifungua kuliko kusubiria mpaka apate uchungu ndo aanze safari ya Kwenda hospital au kituo cha Afya na hata zahanati kitu ambacho kinapelekea kuchelewa kufika na hatimae kupoteza uhai wa mama na mtoto aliyeko tumboni.
Hata hivyo amesema jengo lisikae kama sanamu bali litumike kwaajili ya kusaidia wamama wajawazito na kupunguza vifo visivyo vya lazima jengo hili limejengwa na wafadhili wa Antonius ontwikkelingsfonds kutoka Nchi ya NETHERLANDS
Wafadhili hao wamefanya kazi Tanzania kwa muda mrefu hivyo wakabaini kuwa vifo vya mama na mtoto ni vingi ndo maana waliamua kutoa msaada wa kujenga jengo hilo kwa hospital ya wilaya ya buhigwe ili iwe chachu ya kupunguza vifo hivyo pia amewataka wananchi kujitolea kwa hali na mali kusaidia kwani kutoa ni moyo si utajiri.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz