Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe chini ya Idara ya Elimu Msingi kwa kushirikiana na Program ya shule bora imefanya mafunzo ya somo la hisabati kwa walimu Mahili wa somo la hilo kwa shule za msingi.
Akizungumza Afisa Elimu Taaluma msingi Mabuga Charles amesema kuwa mafunzo hayo yamejumuisha Walimu mahiri wa somo la Hisabati kwa shule zote 94 za serikali zilizopo katika Halmashauri ya Buhigwe.
Aidha ameongezea kwa kusema kuwa dhumuni la mafunzo hayo ni kuwafundisha mbinu mpya ambazo Walimu hao wanaweza kuzitumia ili kuongeza ufaulu wa Wanafunzi katika somo la Hisabati.
Naye muwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo cha Ualimu Tabora Magwija Zakaria amesema kuwa kupitia mafunzo hayo watafundisha mada mbalimbali ikiwemo utumiaji wa Tehama katika ufundishaji wa Hisabati,kutumia zana katika kuifundishia na kutumia mbinu bora katika ufundishaji wa somo la hisabati.
Kwa upande wao Walimu wa somo la hisabati kutoka shule za msingi wamesema kuwa wamefurahia mafunzo hayo na wamejifunza mada mbalimbali ambazo zinaenda kuleta tija katika kutimiza lengo la kuongeza ufaulu wa masomo shuleni.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz