Katika kuzuia na kutibu Magonjwa na Wadudu wa mimea pamoja na kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya Nchi,Wilaya ya Buhigwe imepokea miche safi ya migomba 29,000 Aina ya Mzuzu 4,000 na Kimalindi 25,000 kutoka Wizara ya Kilimo kupitia taasisi ya "Plant Village"inayotarajiwa kupandwa katika mashamba yenye ukubwa wa ekari 32.
Miche hii ni awamu ya nne ikitanguliwa na awamu tatu yenye jumla ya miche 42500,miche 35000 ikipandwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe katika kata za Buhigwe, Mwayaya, Mkatanga, Mubanga, Kibande na Biharu.
Miche ya awamu zilizopita ilipandwa katika jumla ya mashamba 61 yenye jumla ya ukubwa wa ekari 49.5 na kunufanisha wakulima 34, taasisi za shule 14, makanisa 3 na mahakama moja,TaCRI moja na Shamba la jamii moja.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz