Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George E Mbilinyi amewasisitiza program ya Tuungane kuweka misingi imara kuhakikisha miti iliyopandwa inatunzwa.
Akizungumza katika kikao na Tuungane Program leo tarehe 03 Septemba 2024 kilichofanyika ofisini kwake kikiwa na lengo la kufanya tathmini na ufuatilia wa mashamba ya miti yaliyopandwa katika msimu wa mvua kwa mwaka 2023/2024.
Amesema kuwa kama lengo la program linavyosema ikiwemo,utunzaji wa Maliasili hivyo kushirikiana na Halmashauri kuwezesha usimamizi wa sheria ndogo zitakazotatua changamoto ikiwemo ya uchomaji wa moto iliyopo Wilaya ya Buhigwe.
Katika Ziara hiyo ya siku nne kuanzia tarehe 03/10/2024 hadi 06/10/2024 wataalamu wa misitu kutoka Chuo cha Olmotonyi Arusha,SUA,Mizengo Pinda campus,watapima ukuaji wa miti hiyo ili kubaini hali ya ukuaji na pia kubaini kama lengo la utunzaji wa mazingira kupitia upandaji wamiti ya asili kama unafanikiwa.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz