Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewataka Watendaji wa kata za Wilaya ya Buhigwe kuchukua hatua stahiki kwa wanafunzi wenye tabia za utoro pamoja na wazazi au walezi wao ili kukomesha tatizo hilo mashuleni.
Hayo ameyasema leo tarehe 18 Disemba wakati akizungumza katika kikao kazi cha Elimu cha tathmini ya utendaji kazi wa ngazi ya kata za wilaya ya Buhigwe kikiangazia Maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa awali,darasa la kwanza na kidato cha kwanza ikiwemo miundombinu na chakula mashuleni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ndug George Emmanuel Mbilinyi amewataka wasimamizi wote kuongeza uwajibikaji ili kukamilisha miradi mbalimbali ya elimu kwa wakati.
Naye Afisa Elimu Awali na msingi Emmily Fwambo amesema kuwa wamejipanga kukabiliana na changamoto zote ikiwemo kutoa huduma ya chakula cha mchana kwa wanafunzi wote,kutengeneza na kukarabati miundombinu ya shule ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Naye Afisa Elimu Sekondari Onesmo Simime amesema kuwa kwa Idara yake wamejiandaa vizuri kupokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa kuhakikisha miundombinu yote inatengenezwa na kukarabatiwa kwa wakati kabla ya kuanza muhula wa masomo 2025.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz