Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe leo Oktoba 12, 2022 kupitia Mhe. Kanali Michael Ngayalina, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amekiri Halmashauri yake kupokea Tsh. 740,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 37 vya Madarasa. Pamoja na mapokezi hayo Mhe. Ngayalina amepozindua Rasmi ujenzi wa madarasa hayo 37 kwa wilaya nzima
Mapokezi na Uzinduzi huo umefanyika katika Shule ya Sekondari Buyenzi ambapo Viongozi wa Kisiasa, Wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na Waratibu Elimu Kata wameshiriki kusomba matofali kusogeza eneo shule hiyo inakojenga Madarasa matano miongoni mwa 37 yaliyoidhinishiwa pesa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akizungumza kwa upande wa Utendaji Ndg. Essau Hosiana Ngoloka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ameendelea kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kuona elimu inayotolewa inakuwa ni Bora.
Ndg Ngoloka alisisitiza kuwa kwa upande wa watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kabla au ifikapo Novemba 25, mwaka huu ambapo ni siku 5 kabla ya Siku ya mwisho kwa ngazi ya Mkoa na siku 20 kabla ya siku ya mwisho kitaifa ambayo ni Desemba 15.
Mwaka jana Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ilipokea Jumla ya Tsh 1,060,000 kwa ajili ya Vyumba 53 vya Madarasa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimepunguza msongamano madarasani.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz