Ikiwa Leo Juni 5,2024 ni Maadhimisho ya siku ya Mazingira kimataifa Wilayani Buhigwe wameadhimisha kwa kufanya usafi katika maeneo yanayoizunguka Hospital ya Wilaya.
Usafi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mh col Michael Masala Ngayalina na watumishi wa Halmashauri na wananchi wa wilaya ya Buhigwe.
Akiongea katika zoezi Hilo Mkuu wa Wilaya amewashukuru na kuwapongeza watu wote waliojitokeza katika zoezi la kufanya usafi kwa kusema kuwa usafi wa mazingira unapaswa kuwa ratiba ya Kila siku ili kuhakikisha tunaishi katika Mazingira safi na salama.
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Dkt Innocent Mhagama amewashukuru watu wote waliojitokeza katika zoezi la kufanya usafi katika hospital ya wilaya na kuyafanya yaendelee kuwa Bora na ya kupendeza HUDUMA BORA NI FAHARI YETU.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz