Kwa muda wa miaka minne mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe iliopo katika mkoa wa Kigoma yafikia lengo la Mkoa kwa kupata hati safi na hoja saba pekee.
Akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kupitia na kujadili hoja za CAG kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Michael Ngayalina ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kupata hati safi pamoja na hoja chache.
“Nimpongeze Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Venance Kigwinya,Mkurugenzi Mtendaji Ndug George Emmanuel Mbilinyi,Wataalam wote na madiwani kwa usimamisi mzuri hadi kuwa na hoja chache ambayo inafikia lengo la mkoa la kuwa na hoja chache kwa idadi ya tarakimu moja”alisema Mh Kanali Michael
Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Mhe.Hassani Rugwa amewapongeza kwa kuendelea kuvunja rekodi kwa kuwa na hati safi na kuendelea kuwa na hoja chache Zaidi kwa kila mwaka .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe amemshukuru Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma kwa uongozi mwema wenye mchango mzuri wa kuiendeleza Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe pamoja na Mkoa kwa ujumla.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi,Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Erasto Andrew amesema kuwa kuhusu hati iliyotolewa na CAG kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imepata hati safi ikiwa ni muendelezo wa miaka minne mfululizo.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Nje Honest Muya ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa wakaguzi na kurahisisha zoezi la ukaguzi.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mh Robison Mzimya amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Mkurugenzi Mtendaji,Wataalam na viongozi wote kwa uongozi wao imara kwa muda wa miaka mitano ambayo wamekuwa madarakani.
Baada ya kikao hicho Mkurugenzi alitangaza kuvunja rasmi baraza la madiwani lilodumu kwa miaka mitano kufuatia maagizo ya Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Mohammed Mchengerwa kuhakikisha mpaka kufikia tarehe 20 Juni 2025 mabaraza yote ya madiwani kuvunjwa.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz