• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za ofisi |
Buhigwe District Council
Buhigwe District Council

Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo Wa Utawala
    • Idara
      • Utawala Na Utumishi
      • Mipango, Takwimu Na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha Na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Secondari
      • Maji
      • Mifugo Na Uvuvi
      • Ardhi Na Maliasili
      • Maendeleo Ya Jamii Na Ustawi Wa Jamii
      • Ujenzi Na Zimamoto
      • Kilimo,Umwagiliaji Na Ushirika
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi Wa Ndani
      • Habari Na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kiutalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
      • Kuonana na Mhe.Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayotarajiwa Kufanywa
    • Miradi Inayoendelea Kufanywa
    • New Planned Project
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Other Fomu
    • MpangoKazi
    • Baraza-Madiwani
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

BARAZA LA MADIWANI WILAYANI BUHIGWE LAMWONDOA MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO KWA TUHUMA MBALIMBALI ZINAZOMKABIRI

Posted on: June 28th, 2017

BARAZA la madiwani halmashauri ya Wilayani Buhigwe limemuondoa rasmi Madarakani aliekuwa Mwenyekiti wa halmashauri, Elisha Bagwanya kufuatia kuthibitishwa kwa tuhuma mbili kati ya saba zilizokuwa zimewasilishwa kwa tume hiyo zikimkabili Mwenyekiti huyo, moja ikiwa ni kutumia vibaya madaraka na kuisababishia hasara halmashauri .
Uamuzi huo umetolewa leo (28/06/2017) majira ya saa kumi jioni mara baada ya kikao hicho kudumu kwa muda wa masaa matano Katika viwanja vya Shule ya msingi Buhigwe mara baada ya madiwani wa baraza hilo kupiga kura ya ndio kuunga mkono taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa kigoma Brigedia jeneral Emanuel Maganga, iliyokuwa imebaini ukweli wa tuhuma mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani hao na kumtaka mkurugenzi na Baraza kumuondoa Mwenyekiti huyo ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga alithibutisha k kumuondoa mwenywkiti huyo kwa kutangaza matokeo ya kura 20 za ndio na saba za hapana zilozo pigwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo .
Mkurugenzi Mtendaji akiwasilisha taarifa ya Tume kwa Waheshimiwa Madiwani kwaajii ya MajadilianoNyamoga alisema mnamo tarehe 25 machi alipokea barua kutoka kwa madiwani 20 wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wa halmashauri na kwamujibu wa kanuni Na 4(3) ya kanuni za kudumu za Halmashauri wajumbe wa Mkutano wasiopungua theluthi mbili wanaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano kwa lengo la kujadili agenda ya kumuondoa madarakani mwenyekiti wa halmashauri kutokana na sababu zinazotajwa, na tuhuma zilizo tajwa katika barua hiyo ni tuhuma saba na moja wapo ikiwa ni kutumia madaraka ya uongozi vibaya kwa kutumia trekta ya halmashauri kulimia shamba lake.
Alisema tume ya mkuu wa mkoa baada ya kupitia tuhuma zote saba zilizotajwa katika barua hiyo ilibaini tuhuma mbili ni za ukweli na zinamnyima Mwenyekiti huyo sifa za kuwa kiongozi, tuhuma hizo ni pamoja na kufanya kazi ya ukandarasi na halmashauri kwa kutumia kampuni yake inayoitwa BUYENZI GENERAL SUPPLIES kwa kazi ya mradi wa maji Nyamugali ambao ni mbovu ,mradi wa Barabara ya Kijiji cha Kigogwe Mrungu kujenga mradi huo kwa kutumia kampuni ya NGELUKE CONSTRUCTIONS kwa kutumia uwezo wake kama mwenyekiti wa halmashauri na kuzuia miradi hiyo isikaguliwe.

Alisema Kuthibitika kwa tuma hizo mbili zinamuondoa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa Mwenyekiti na halmashauri hiyo ya Buhigwe inaungana na Mkuu wa Mkoa kumuondoa madarakani kutokana na ukiukwaji wa kanuni alioufanya Mwenyekiti huyo, ilikuhakikisha halmashauri hiyo inapata kiongozi mwingine na inaemdelea na majukumu yake.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marco Gaguti kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa aliwaomba madiwani hao kuweka mbele masilahi ya Wananchi walio wachagua ilikuhakikisha haki inatendeka na halmashauri inakuwa salama kwa kupata Viongozi waadilifu na wanaozingatia maadili ya uwajibikaji na kuwatumikia Wananchi.

Kwaupande wake aliekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elisha Bagwanya alisema yeye kwaupande wake alijitoa katika kampuni ya BUYENZI GENERAL SUPPLIES tangu mwaka 2011 na katika tuhuma hizo saba hakuna tuhuma hata moja inayo muhusu , kuanzia alipoingia madarakani hakuwahi kuomba kufanya kazi yoyote katika halmashauri hiyo na haoni sababu ya yeyekuondolewa katika nafasi yake.
Mh. Mwenyekiti akitowa utetezi wake kabla ya Maamzi ya Madiwani Kumng'owa wadhafa wakeAlisema tatizo linalojitokeza ni baadhi ya madiwani wenzake kuwa na uchu wa madaraka na kupanga kumiondoa katika nafasi yake na kwamba yeye hanatatizo loloye na anastahili na
Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo mara baaada ya kupokea taarifa ya tume ya Mkuu wa Mkoa waliionyesha kutolizishwa na uamuzi huo na baadhi a akiwemo diwani wa kata ya Kajana Robisoni Ngeze waliafiki maamuzi hayo , alisema wao wanaunga mkono maamuzi ya Mkuu wa Mkoa na tuhuma hizo ni za kweli tume iliyoundwa haiwezi kusema uongo na hawawezi kuwa na uchu wa madaraka yake na kwamba maazimio yaliyotolewa ni mazuri na yanaungwa Mkono na Baraza.
Alisema Baraza la madiwani linaushahidi na tuhuma hizo kwamba mwenyekiti huyo aliwahi kuwaomba madiwani wasiende kukagua mradi huo wa Maji na barabara awapatie fedha na madiwani waligoma na kudai lazima miradi hoyo ikaguliwe, tuhuma hiyo inatosha kiwa mwenyekiti huyo hafai kuwa katika kiti hiko.
Hata hivyo mwenyekiti ya tume ya uchunguzi ya tuhuma zinazo mkabili Mwenyekiti wa halmashauri Moses Msuluzya alisema tume ilichunguza na kubaini tuhumba mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani, alisema mwenyekiti aliandika barua ya kuondoka katika kampuni hiyo na mwaka 2015 aliandika barua kwa siri ya kuomba kurudi katika kampuni, na baada ya kustaafu udiwani aliomba fedha yake ya kiinua mgongo iingizwe katika kampuni ya Buyenzi na kudai yeye ndiye mtia saini pekee katika kampuni hiyo.

Alisema vielelezo hivyo vilitosha kuonyesha kuwa tuhuma hizo ni kweli na hapaswi kiendelea kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wameamua kumuondoa na halmashauri itaendelea na mchakato wa kumpata mwenyekiti atake wajali na kuwatetea wananchi bila kujali maslahi yake.

Wananchi wa halmashauri hiyo, akiwemo mzee Yasini Kandaga alisema anawashukuru sana madiwani kwa kuamua kumuondoa Mwenyekiti huuo, alikuwa akitumia madaraka yake vibaya na kupelekea kuzolotesha maendeleo ya wilaya hiyo na kuwanyanyasa wananchi kutokana na uongozi aliokuwanao.

Alisema serikali ya sasa ni serikali inayowajali wananchi nakuwaomba madiwani kutenda haki na kuchagua mwenyekiti mwingine ambae ni mwadirifu na atakae kuwa na maono ya kuibua miradi itakayo weza kuinua uchumi wa Wananchi wa Wilaya hiyo

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI - 04.07.2023 June 23, 2023
  • KILA KHERI DARASA LA SABA September 12, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA - OKTOBA 2023 October 09, 2023
  • TANZIA February 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED BUHIGWE ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA.

    May 05, 2025
  • MATOKEO 2024 WALIMU NA WANAFUNZI WAPONGEZWA.

    April 17, 2025
  • BABA ASKOFU EMMANUEL BWATA AITIKIA WITO WA MKURUGENZI BUHIGWE.

    April 14, 2025
  • SHEREHE YA KUWAAGA WATUMISHI NA KUWAKARIBISHA WATUMISHI BUHIGWE YAFANA.

    April 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe kuanza kutoa huduma za Afya
Video Zaidi

Kurasa Za Karibu

  • Kuhamisha Mwanafunzi
  • Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep Documentation
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • Wahe. Madiwani
  • BEMIS

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Bunge La Tanzania
  • Ikulu
  • Bodi Ya Manunuzi na Ugavi
  • Wizara ya Ardhi
  • Wizara ya Elimu, Sayansi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi

    Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe

    Simu Ya Mezani: 0282988460

    Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333

    Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Mwanzo

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Buhigwe. Haki zote zimehifadhiwa