Akizungumuza wakati wa kikao maalamu cha baraza hilo katika Ukumbi wa Halimashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mh Venance S Kigwinya Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo amesema rasimu hiyo ya bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 32.7 itasaidia na kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii kama vile huduma za Sekta ya Elimu, huduma za Afya, maendeleo ya jamii, mazingira, ambapo katika rasimu hiyo kiasi cha shilingi. Bilioni 10,6 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za miradi ya maendeleo.
Hata hivyo baraza hilo la madiwani limepokea na kuidhinisha taarifa ya rasimu ya bajeti ya taasisi ya TARURA kiasi cha shilingi billion 3.9 ikiwa lengo ni kuboresha na kupendekeza miradi ya barabara itakayotekelezwa na taasisi hiyo katika halmashauri yetu. Pia baraza hilo limeishukuru taasisi hiyo kwa kuona ni vema baraza kutoa baraka katika rasimu ya bajeti hiyo na kuwaomba endepo bajeti hiyo itaidhishwa rasmi kwa matumizi basi miradi pendekezwa itekelezwa kwa ukamilifu
Mhe, Venance S Kigwinya ameeleza kwamba Baraza la Madiwani halitokuwa tayari kumvumilia Kiongozi ama mfanyabiashara yeyote atakayesababisha na kuleta ukwamishaji katika suala la Ukusanyaji wa Mapato kwa kuzingatia kuwa kipaumbele cha Halmashauri ya Wilaya ya buhigwe ni Kuboresha usimamizi wa vyanzo vya mapato ya ndani na kuibua vyanzo vipya kwa lengo la kuwaletea maendeleo Wananchi wa Wilaya hiyo.
Bi, Utefta Mahega katibu tawala wa wilaya hiyo amesema kwamba Baraza la Madiwani lina wajibu wa kusimamia mapato ya ndani kwa bidi kwa maslahi mapana ya Wananchi na kuhakikisha kutokutoa mwanya wa upotevu wa mapato kwa namna yeyote ile na kuwataka Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia na kutumia kikamilifu fedha za Miradi ya Maendeleo katika Kata zao vizuri,
Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti ya mwaka 2024/2025 Afisa Mipango Bw.Bryton Pomo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya buhigwe amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha Bilioni 1.5 ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha shilingi. Bilioni 19.7 ni fedha ya mishahara ya Watumishi,kiasi cha shilingi Bilioni 1.07 ni ruzuku ya uendeshaji wa ofisi ( OC) na kiasi cha Bilioni 10.6 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na fedha zote ni kutoka Serikali kuu.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Alphonce I Haule amesema Bajeti hii ya mwaka wa fedha 2024/2025 ni lazima itatekelezwe kwa kuchukua hatua madhubuti katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na fedha zitakazotoka Serikali kuu kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya maendeleo, zitasimamiwa vizuri kwa maslahi mapana ya Wananchi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz