Faida za elimu ya Kujitegemea zilizopatikana Katika shule ya Msingi Kibwigwa. Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe
Jumla ya miradi nane (8) yenye thamani ya shilingi 672,790,000 imetembelewa na mwenge wa uhuru mwaka huu 2018. Aidha, Serikali kuu imechangia shilingi 533,290,000 sawa na 79%, Halmashauri shilingi 17,500,000 sawa na 3%, Wahisani shilingi 50,000,000 sawa na 7% na Wananchi shilingi 72,000,000 sawa na 11%.