Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Ndug Hamza Seif Mnaliwa amewaasa makarani waongozaji Wapiga kura kuzingatia sheria,kanuni na maelekezo watakayopewa hadi kukamilika kwa jukumu la Uchaguzi mkuu.
Ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya makarani waongoza wapiga kura,wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo yaliyoanza leo tarehe 25 oktoba hadi tarehe 27 Oktoba 2025 watakaosimamia uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 oktoba mwaka huu.

”Dhamana mliyopewa ya kusimamia zoezi la uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wabunge na madiwani kwa Tanzania bara ni kubwa,hivyo mnategemewa kuzingatia sheria,kanuni na maelekezo mtakayopewa hadi hapo tutakapokamilisha jukumu hili la Uchaguzi mkuu”alisema Mnaliwa
Ameongeezea kwa kuwasihi kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kufanikisha Uchaguzi katika vituo watakavyopangiwa.

Makarani hao wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo majukumu yao wakati wa zoezi la uchaguzi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz