Tarehe 23/12/2021 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Buhigwe Ndg. Essau H. Ngoloka alifanikiwa kuziunganisha na kusimamia makabidhiano ya familia mbili(Familia iliyoibiwa mtoto Mkoa wa Mpanda na Familia ya kuaminika ambayo ilikubari kumtunza mtoto hapa Buhigwe bada yakutelekezwa na kuopatikana Kitambuka). Aidha, tukio la uwizi wa mtoto lilifanyika Mkoani Mpanda Wilaya ya Simbo mwezi Septemba 2021 na mtoto kupatikana kijiji cha Kitambuka Wilaya ya Buhigwe mara baada ya kutelekezwa na Mwizi huyo mwezi Novemba 2021. Jeshi la polisi kwa ushirikiana na ofisi ya Ustawi wa Jamii mwezi Decemba 2021 walishirikiana kuhakikisha mtoto huyu wazazi wake wanapatikana na anaunganishwa na wazazi wake. hata hivyo mtuhumiwa baada ya kutelekeza mtoto hajapatika wala kubainika aliko.Pamoja na mambo mengine baada ya makabidhiano hayo. Mkurugenzi Mtendaji (W) alisisitiza wananchi kuendelea kujiepusha na vitendo vya ukatili kwa watoto, Kuwalinda, kuwa makini katika malezi ya watoto, kuepuka kuwapokea watu wasiojulika bila taarifa pamoja na wananchi kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili kwa watoto ili Hatua za kisheria zichukuliwe.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz