Mkuu wa Wilaya Buhigwe Col Michael Ngayalina ameelaani vikali tabia ya baadhi ya watendaji katika sekta ya afya kushidwa kufaya kazi kwa kuzingatia maadili na miongozo ya kazi zao na kusababisha kuharibu taswira nzuri ya taasnia hiyo kwa jamii.
Col Ngayalina ametoa kauli hiyo alipozugumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika kiwilaya katika hospitali ya wilaya ya Buhigwe na kusisitiza kuwa maadhimisho yanalenga kutafakari na kubaini thamani na mchango mkubwa wa sekta hiyo katika kuhakikisha utimamu wa afya kwa jamii.
Ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya kwa jamii siku ya wauguzi inachagizwa na kutambua mchango mkubwa wa wauguzi katika kupunguza vifo vya wajawazito na Watoto wachanga , malaria kifua kukuu ,polio kufubaza virusi vya ukimwi sanjari na kuyakabili maradhi mbalimbali.
Sambamba na hayo muuguzi mkuu wa halmashauri ya wilaya Buhigwe Bi Jenipha Raymond amezitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo kuwa ni kutotosheleza kwa ikama ya watendaji , mazingira magumu ya utendaji kazi kwa aadhi ya maeneo kukosa ufadhili wa uhakika kujiendeleza kitaaluma Pamoja na kutotosheleza kwa vifaa tiba na utoaji huduma isiyo na ubora
Hafla hiyo imehudhuriwa na katibu tawala wilaya Mkurugezi Mtendaji Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya Mganga Mkuu Wilaya na wananchi
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz