Shukurani hizo zimetolewa katika mwendelezo wa ziara ya Mhe Katibu Tawala Mkoa wa iKgoma kwa Wilaya ya Buhigwe.
Hata hivyo hayo yamesemwa na baadhi ya wagonjwa walioenda kupata huduma za matibabu katika Zahanati ya LEMBA ambayo imefunguliwa rasimi Leo 01/03/2024 na kuanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi hao.
Akizungumza mmoja wa wagonjwa hao amesema kuwa upatikanaji wa huduma za matibabu katika Zahanati hiyo kutapunguza usumbufu waliokuwa wakiupata hapo awali kwa kutembea mwendo mrefu Sana kufuata matibabu hayo.
Pia wamesisitiza jamii kuachana na Imani potofu za kishirikna na badala yake waende katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kupata vipimo na matibabu yaliyosahihi.
Pamoja na hayo wamesema utakuta mtu anasumbuliwa na tezi dume hususani kwa wazee wa zaidi ya miaka 60 lakini hataki kwenda hospital kupatiwa matibabu na ikitoa akaaga Dunia wanasema ameuliwa kwa Imani za kishirikna.
Wakati hayo yakiendelea wamemshukuru Mh Rais Dkt; SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwajali na kuwakumbuka kwa kutoa Fedha za miradi mingi Sana inayotekezwa Wilayani Buhigwe Mwenyezi Mungu azidi kumbariki.zaidi na zaid
Mhe.Msovera amewakata timu ya menejimenti kusimamia miradi ipasavyo na Ile ambayo walitoa ahadi ya kuikamilisha ikamilike kwa muda waliosema na kuanza kutoa huduma mara Moja.
Miradi iliyokaguliwa ni Zahanati ya LEMBA kasumo kituo Cha Afya kajana hospital ya wilaya nyumba ya mkurugenzi na uzio wa Halmashauri.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz