Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe wameshauriwa kutumia Wiki ya Sheria kwa ajili ya kupata haki zao.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina leo tarehe 25 mwezi Januari mwaka 2025 wakati akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa Wiki ya Sheria kwa Wilaya ya Buhigwe ambayo imeanza tarehe 25 na kilele tarehe 3 mwezi February kwaka huu.
“Asubuhi ya leo tumekusanyika,tumepanda miti ya kumbukumbu na kutembea kwa pamoja kuzindua wiki ya sheria kwa Wilaya ya Buhigwe,kuna wataalamu ambao watatoa msaada wa kisheria kwa wiki hii yote hivyo nitoe rai kwenu Wananchi tutumie wiki hii kupata msaada wa kisheria ili tupate haki zetu”Alisema Kanali Michael
Aidha amewaasa kutumia mahakama kama sehemu ya msaada na kuacha kuogopa kufika inapofika suala la kutafuta haki
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi ameipongeza Mahakama ya Wilaya kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kuhusu Wiki ya kisheria na kuwaasa Wananchi kutumia wataalamu hao kupata haki zao.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Buhigwe Katoki Venancy Mwakitalu amesema kuwa maadhimisho hayo ni ya awamu ya tatu tangu ilipozinduliwa Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe mnamo mwaka 2022 na kwa mwaka huu wa 2025 yamezinduliwa rasmi na matembezi maalumu huku Mahakama ikiendelea na kutimiza dira yake ya utoaji haki kwa wakati na kwa watu wote.
Naye Wakili Gaudensia Mdaki kutoka Wizara ya sheria na katiba amewakaribisha Wananchi wote wenye migogoro kwa ajili ya kupata ushauri na msaada wa kisheria.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz