WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA H/W BUHIGWEWAMEFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KATIKIA H/W HIYO
Posted on: December 28th, 2022
Mkuu wa wilya ya buhigwe Mhe. KANALI MICHAEL MASALA JUSTIN NGAYALINA akiongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wamekagua miradi ambayo inatekelezwa kwa force account
Miradi iliyokaguliwa ni soko la kimkakati mnanila, kituo cha afya mwayaya, kituo cha afya kajana, shule ya wasichana kahimba, bweni la watoto wenye mahitaji maalumu shule ya msingi muyama,shule ya sekondari katundu, hospitali ya wilaya ,ukumbi wa halimashauri, nyumba kumi za wakuu wa idara, na mgahawa
Aidha ujenzi wa soko la kimkakati la mnanila linalenga kuiongezea halimashauri mapato na pia kuwanufaisha wanachi wote kwa kuwa na maeneo mazuri na bora ya biashara amabapo ujenzi huo unagharimu kiasi cha tsh 600,000,000/= mpaka kukamilika
Hata hivyo kwa upande wa afya majengo hayo yanalenga kuboresha huduma za afya kwa wanachi pia kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifunga na huduma bora za upasuaji na magojwa mangineyo
Katika kuhakikisha suala la elimu linapewa kipaumbele wilaya ya buhigwe imepata fedha za kuboresha na kujenga madarasa ili kusaidia watoto kupata elimu katika mazingira bora kwa afya zao
Upande wa shule za sekondari halimashauri ya wilaya ya buhigwe imepata fedha za kujenga shule ya wasichana ya kidato cha tano na sita ambayo iko hatua mbalimbali za umaliziaji wa madarasa mabweni vyoo nyumba za walimu, bwalo, na upandaji wa miti, matarajio shule hiyo ianze kupokea wanafunzi july 2023
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama imepongeza jitihada za wasimamizi wa miradi na kuwataka waongeze kasi zaidi ili kukamilisha miradi kwa muda uliopagwa na matumizi yake yaanze mara moja