Mhe. Col. Michael Nhayalina, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe ametoa msaada wa chakula na blanketi kwa wahanga wa kimbunga katika vijiji viwili ambavyo ni kitambuka na kibwigwa ambapo kaya zipatazo 16 zimepata maaf aya kuezuliwa na kuboka kwa nyumba kumia na sita zilizosababishwa na kimbuga kilichoambatana na upepo mkali na mvua kubwa
Maafa hayo yalitoke siku ya ijumaa tarehe 13/01/2023 muda wa saa saba mchana katika tarafa ya manyovu kata ya mkatanga kijiji kitambuka na kata ya kibigwa ambapo mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuathiri makazi ya wananchi wa vijiji hivyo hali iliyosababisha hara kubwa kwa jamii hizo ikiwemo baadhi yao nyumba kuezuliwa na kubomoka kabsa na kusababisha kukosa makazi ya kuishi licha ya wasamalia wema kujitolea kuwapa makzi kwa sasa
Aidha mkuu walaya ya buhigwe akiongea na wahanga hao katika uwanja wa shule ya sekondari kitambuka amewapa pole pia salamu za pole kutoka kwa mh. Dr samia suluhu hassani raisi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania na kuwomba wahnaga hao kupokea hicho kidogo ambacho amabcho anaenda kukiwasilisha kwao
Pia amewaasa kusema kwa pamopja matatizo waliyonayo wanajitahidi watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza waende shule kwa muda uliopangwa na sekali asiwepo hata mmoja ambambaye hataenda shule hatua kali zitachukuliwa na serikali kuhusu suala hilo
Baada ya hayo yote mkuu wa wilaya ya buhigwe pamoja na timu yake yote aliyoambatana nayo akishilikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilayani buhigwe,waheshimiwa madiwani ,wenyeviti na viongozi mbalimbali wa kata wamekabidhi unga wa sembe kg 25,mifuko 16,blanketi 16, maharage kg 70 kwa wahanga wa tukio hilo
Hata hivyo baada ya makabidhiano mkuu wa wilaya alitembelea nyumba zote zilizopata matatizoili kujionea uharibifu uliofanyika katika kaya hizo. Pia viongozi wa viji na wananchi waliogiswa na matukio hilo pia walitoa michango yao kusaidia wahanga hao ambapo kamati za maafa za vijiji hivyo walichangia kiasi kiasi cha shilingi laki mbili na elfu tisini mia tano kwa kijiji cha kitambuka ambapo miasaada yote hiyo imeshakabidhiwa kwa waathirika
Shukurani za dhati ziende kwa Mhe dr Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mungu azidishe pale alipotoa pia awe na moyo huohuo wa kusaidia watu wote wenye matatizo hayo ni maneno kutoka kwa wahanga.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz