Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilayani Buhigwe ndugu Peter N. Masindi amewaasa wafanya biashara wilayani humo kuchangamkia fursa za uwekezaji ili kujikwamua katika wimbi la umaskini.
Hayo yamesemwa katika kikao cha Baraza la Biashara kilichofanyika katika ukumbi wa Champanda wilayani hapa mapema wiki hii.
"Nawaasa kuchangamkia fursa za uwekezaji hasa kwa mazao ya Kahawa, Michikichi na Migomba ili kupiga hatua na kuwa wafanya biashara wakubwa nchini na hata nje ya nchi badala ya kutegemea biashara ya vibanda tu" Aliongeza Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara.
Makaumu Mwenyekiti alitumia fursa hiyo kuwapongeza wajumbe wa Baraza la Biashara kwa kuhudhuria kikao hicho na kutoa maoni ambayo yatasaidia kujenga Buhigwe mpya yenye ushindani wa kibiashara.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz