Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi amewataka viongozi wote wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa Novemba 27 mwaka 2024 kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na kanuni za Nchi ili kupata matokeo chanya katika taifa.
Ameyasema hayo leo hii tarehe 03 mwezi Januari mwaka 2025 katika Mafunzo Elekezi ya kiutendaji kwa Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji,pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji.
Aidha amewataka viongozi hao kutumia mafunzo waliyopewa kama muongozo katika kutekeleza majukumu yao na kuwasisitiza kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika shughuli zap za kila siku na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz