Taasisi ya DORIS MOLLEL FOUNDATION inayojitolea kusambaza na kugawa Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto waliozaliwa Njiti Nchini na Kampeni yao ya WATOTO NJITI WANAISHI imetoa Vifaa tiba vyenye thamani ya Jumla ya Tsh. Mililioni 190 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kwa kushirikiana na ORYX GAS pia imetoa jumla ya Mitungi 300 kwa ajili akina mama wajawazito ili kupunguza hatari ya kuzaa watoto njiti kwa kutumia Nishati salama kupikia.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi. Doris Mollel amesema ameona umuhimu wa kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kuokoa vifo vya watoto Njiti Wilayani hapa ambapo kwa mwaka 2022 jumla ya Vifo 24 vilirekodiwa vikitokana na watoto kuzaliwa chini ya uzito.
Taasisi hiyo kwa Kushirikiana na Taasisi ya Uturuki ya C.TIKA pia imetoa Madawati 450 kwa ajili ya Shule mpya ya Kahimba.
Mgeni Rasmi katika Shughuli hiyo Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuchukulia jambo hilo kwa uzito mkubwa
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz