Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Bw Anosta Nyamoga, akishiriki vyema kwenye uzinduzi wa uandaaji wa udongo kwa ajili ya kufyatua matofali ambayo yatatumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Munzeze. katika uzinduzi huo, mkurugenzenzi alihamasisha kujituma kwa kuonesha moyo na ari kama ambavyo walifanya siku ile na kuzidi kuleta maendeleo wilayani.
Mkurugenzi mtendaji aliwaeleza wananchi kuwa maendeleo yao hayana itikadi na hayachagui, hivyo wajitume na serikali haiko mbali nao na haitoacha kuwaletea miradi ya maendeleo. hata hivyo aliomba wananchi wa sehemu zote katika halmashauri yake kuiga mfano wa wananchi wa kata ya Munzeze kwa juhudi walizozionesha
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz