Uongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya Buhigwe Mkoani Kigoma Ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mhe. Kanali Michael Ngayalina, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe Mhe. Alphonce Haule, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndg. Venance Kigwinya pamoja na Baraza la Madiwani wamefanya ziara katika Wilaya ya Mufindi shamba la miti Saohill na Kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Dkt Linda P Salekwa ili kujifunza shughuli za uhifadhi wa misitu na zinavyofanyika katika shamba hilo.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Ngalina ameanza kutoa shukrani zake kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuendeleza uwekezaji kwa Wakala wa Huduma za Misitu ‘TFS’ Tanzania ili kuendeleza uhifadhi na kuchangia katika upatikanaji wa mapato yatokanayo na mazao mbalimbali ya misitu.
Amesema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania-TFS ili kuhakikisha wanafanikisha lengo la kuja kujifunza shughuli za uhifadhi.
"Kwa namna ya Pekee nipende kumshukuru Kamishna wa Uhifadhi Prof. Dos Santos Silayo ambaye alitembelea Wilaya yetu na baada ya kuona chamgamoto tunazozipata alitualika ili tuweze kufanya ziara hii pamoja na Waheshimiwa madiwani" amesema.
Ameongeza kuwa katika wilaya ya Buhigwe ina hali ya hewa inafanana na na eneo la wilaya ya Mufindi lakini pia wana maeneo mengi ya wazi ‘vipara’ ambayo yanafaa kupandwa miti na kuendeleza dhana ya Uhifadhi na kupata mapato kama ilivo huku.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe Alphonce Haule ameipongeza TFS kwa kazi inayofanya na kusema wamejifunza vitu vingi kutoka Saohill ikiwemo uhifadhi wa misitu na utunzaji wa mazingira.
" Tumepita kwenye vitalu vya kuzalisha miche
na tumeona jinsi inavyoandaliwa na tumegundua kwamba sisi kama Halmshauri ya Buhigwe tunayo nafasi ya kuanzisha shamba letu ambalo litakuwa ni mojawapo ya chanzo cha mapato"
Aidha ameongeza kuwa kama halmashauri wanayo nafasi ya kukaa pamoja na uongozi wa TFS Buhigwe na kuona uwezekano wa kuwaongezea eneo lingine sababu eneo lililopo kwa sasa ni dogo.
Mhe. Elesi Elia Gwoma ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa upande wake anaipongeza na TFS kwa jazi inayofanyika ya Uhifadhi. Amesema kama halmshauri wamepata elimu kubwa ambayo itawachagiza na wao kufanya uhaifadhi kama walivyoona kutoka katika Shamba la miti Saohill. Ameongeza kuwa huko Buhigwe hata wao wanayo misiti lakini hawapo kwenye hatua kama waliyojifunza hapa hivyo nao watafanya juhudi ili kufika juu zaidi.
Naye Hassan Katura Diwani kata ya Kilelema amesema kuwa wao kama wadau wa mazingira watakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kusisitiza uhifadhi wa misitu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na hata cha baadae.
" Ziara hii ni zaidi ya Shule kwetu, hivyo madiwani kama wadau wa misitu pia naamini watakwenda kuboresha mazingira wanayoyaongoza" amesema.
Katika Ziara hiyo Wageni hao waliongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill PCO Tebby Yoramu akiambatana na Mhifadhi Msaidizi SCO Said Singano, Mhifadhi kutoka Shamba la miti Bihigwe, Mhifadhi wa tarafa ya Kwanza pamoja na Afisa Maliasili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufundi Gilbert Ngailo.
Ziara hiyo iliendelea kwa Siku ya Pili ya Tarehe 29.08.2023 kwa Wah. Madiwani na uongoiz kutembelea Viwanda vitatu vinavyozalisha thamani na vitu kutokana na malighafi za Miti kama Mkaa mbdala, Venia, Fenicha nk na baadae walitembelea Eneo unakofanywa utafiti wa Uvunaji wa Utovu wa Miti hiyo kabla ya Kuvunwa
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kupata mlo wa Pamoja ambapo mwisho PCO aliwashukuru na kuwakaribisha tena ana kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Venance Kigwinya ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri alitoa shukrani kwa kuwakaribisha Menejimenti ya Saohill kuja Buhigwe huku akisistiza kufanya kwa vitendo mazuri waliyopata hapo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz