Hayo yamesemwa leo katika kikao kazi cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wanawake na watoto (MTAKUWWA)ngazi ya mkoa kilichofanyika ukumbi wa Hospitali ya wilaya ya Buhigwe majira ya saa 3 asubuhi.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto ngazi ya wilaya, Afisa Ustawi wa Jamii (w) Bwana Petro Mbwanji amesema kamati inaendelea kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto sanjari na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ukatili wa wanawake na watoto na athari zake.
Aidha kamati ya MTAKUWWA (w) imetoa mafunzo kwa kamati za ulinzi na usalama wa wanawake na watoto ngazi za kata na vijiji vyote 44 vya wilaya ya Buhigwe, hata hivyo yapo mashauri ambayo yameondolewa mahakamani na mengine watuhumiwa wamehukumiwa jela.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoa Bw. Jonas Joas akijibu taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa na Afisa Ustawi wa Jamii (w) amesema pamoja na majukumu ya kamati hiyo ni vizuri kuhakikisha kwamba watoto wote wenye umri wa kwenda shule na walioko shule wanahudhuria masomo bila kubughudhiwa wala kuwa watoro na walau kuwe na mlo mmoja tena wenye viazi lishe shuleni . Joas aliendelea kusisitiza juu ya clubs za watoto shuleni kwamba zinapaswa kuwa na tija ili zitusaidie kuibua vitendo vya ukatili, mojawapo ya club ilyoanzishwa na mradi wa EQUIP Tanzania ni "JUU club" yaani Jiamini uwezo unao. Pia kamati ijikite kwenye upimaji wa mimba kwa watoto wa kike shuleni na kupunguza masoko ya usiku hasa kwa watoto wa kike ambao ndio wahanga wakubwa.
Naye kaimu Katibu Tawala Mkoa Mhe.Moses D. Msuluzya ametoa wiki mbili kwa kamati ya MTAKUWWA (W) kuwatafuta wazazi na watoto ambao ni watoro ili kutambua sababu za kutokuhudhuria masomo na ni hatua gani zimechukuliwa dhidi yao. Pia viongozi wa dini msihamasishe suluhu dhidi ya vitendo vya ukatili bali kemeeni waumini wajiepushe na ukatili wa aina yoyote kwakuwa sheria haijakaa kimya.
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Simon Chacha naye hakubaki nyuma kwa kushauri kuwepo kwa jengo la" One Stop Center" ili kuharakisha uamzi wa vitendo vya ukatili kwakuwa kesi nyingi za ukatili zinaishia ngazi ya jamii kiholela, pia kamati ya MTAKUWWA (W) hakikisheni swala la utumikishwaji wa watoto katika maeneo mbalimbali kama mashambani na maeneo ya ufyatuaji tofali yanakomeshwa na wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Hakimu Mkazi wa Mkoa Kigoma Mhe. Gadiel Mariki ameshauri waongezwe waendesha mashataka na OCCID(W) kwenye kamati ya MTAKUWWA na shauri l isichukue muda mrefu kufanyiwa uamzi ndipo matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yatakoma.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Kigoma amesema elimu ya vikundi vya wanawake na vijana iendelee kutolewa ili walengwa wanufaike na pesa inayotolewa na serikali.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji (w) Buhigwe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya MTAKUWWA ngazi ya wilaya amewashukuru kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa na kuahdi kuyafanyia kazi yote yaliyoshauriwa lengo likiwa ni kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz