Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imekagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya wenye gharama ya Tsh. 2,224,708,500 sawa na 90.8% ya Bajeti ambapo kiasi cha Tsh 1,852,428,962 sawa na 33.76% kimeshalipwa.
Ziara hiyo imefanyika mapema leo asubuhi eneo la Bwega wilayani hapa ambapo imeongozwa na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri Venance Kigwinya. Akizungumza katika ziara hiyo Kigwinya amesema ujenzi ukamilike kwa wakati ili kutoa huduma kwa wananchi.
"Tunakagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi huu wa Hospitali dhumuni kujiridhisha fedha ya Serikali iliyotolewa na kujua mradi jinsi unavyoendelea". Amesema Kigwinya
Kutoka kulia ni Mhe. Costa Mbaya Diwani wa kata ya Nyamugali, akifatiwa na Mhe. Nzeye Andrew Nimubandi kata ya Kibwigwa, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Venance Kigwinya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Elihuruma Nyella na Mganga Mkuu wa Wilaya Ndg. Deus Ruta.
Kwa upande wake Mhandisi wa Wilaya Bwana Aidan S. Ngatomela amesema mpaka kufikia tarehe 30/9/2019 ujenzi huo utakuwa umekamilika licha ya changamoto zinazokabili ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mhandisi wa Ujenzi (W) Bwana Aidan S. Ngatomela akiwaonesha wajumbe wa kamati ya fedha, uongozi na mipango jengo la wodi ya wazazi, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz