Kamati ya Fedha , Uongozi na Mipango inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Buhigwe Mh.. Venance Kigwinya (wapili kushoto) imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri hiyo , muhandisi wa Wilaya Bwana Aidan (Aliyenyanyua mkono) akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa Shule ya mfano Bwega kama inavyoonekana katika picha.
Kamati hiyo imetembelea mradi wa shule ya mfano Bwega na kukagua majengo mbali mbali yakiwemo majengo ya madarasa, vyoo , maktaba nyumba za walimu pamoja na bwalo na kulizishwa na kasi ya utekelezwaji wa mradi huo ambao upo katika hatua mzuri.
Aidha kamati hiyo imetembelea pia Mradi wa Soko la kisasa lililoko eneo la Munanila na kukagua ujenzi wake ambao bado unaendelea , na kushauri nguvu iongezwe ili soko hilo liweze kutumika kwa wakati na kusaidia wananchi wa eneo hilo ili liwe chachu ya maendeleo katika eneo la Munanila wilayani Buhigwe.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz