Akizungumza katika kikao cha maelekezo kwa wakuu wa shule za zote za SEKONDARI kilichoitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe juu ya usimamizi wa mradi wa ujenzi wa madarasa unaoendelea Buhigwe, Mkuu wa wawilaya hiyo(Buhigwe) Kanali Michael Ngayalina amewataka wakuu wa Shule kuwa na umakini wa hata zaidi ya asilimia mia ili kuwezesha kukamilisha miradi hiyo kwa ubora na ufanisi. Pamoja na hayo
Pia mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Ndg. Venance Kigwinya amesisitiza UBORA katika ujenzi huo ili kukwepa sura chafu ya halmashauri ambayo ilikuwepo hapo awali kwa sababu ya ujenzi wa baadhi ya miradi chini ya kiwango.
Mwanzoni akifungua kikao hicho mkurugenzi mtendaji Bwana Essau Ngoloka ametoa maelkezo na mwongozo utakaofuatwa katika kukamilisha ujenzi huo wa madarasa
Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe ilipata jumla Tsh 1,060,000,000 kwa ajili ujenzi wa jumla ya madarasa 53
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz