Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ambao ni Wanachama, wapenzi na washabiki wa Klabu ya Mpira wa Miguu SIMBA SC wamekabidhi Jumla ya Mifuko 46 ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya Kirungu na Kasumo wilayani hapo yenye dhamani ya Jumla ya Tsh. 1,093,000/=
Akikabidhi Mifuko hiyo kwa Ndg. Essau Hosiana Ngoloka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe, mwakilishi wa Wanasimba hao Ndg. Erasto Endrew amesema wanaendelea kuonesha Ushabiki wao kwenye maendeleo yanayoonekana nje ya ushabiki wa maneno na vijiweni.
Ndg Erasto ameendele kusisitiza kuwa Simba ni moja na wamoja na watahakikisha wanashinda uwanjani, na katika suala la maendeleo kwa kauli ya WE WIN TOGETHER, WE LOOSE TOGETHER AND WE DRAW TOGETHER, SIMBA NGUVU MOJA.
Huo ni muendelezo wa wananchama hao kufanya kwa vitendo nje ya ushabiki kwa ajili ya maendeleo; Awali Washabiki na wananchama hao walikabidhi mifuko 23 katika kwenye kata ya Kajana.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz