Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameongoza maelfu ya wakazi wa Buhigwe kusherehekea Miaka sitini ya Uhuru wa Tanganyika kwa kupanda miche ya Chikichi katika shule ya Sekondari Bwafumba iliyoko kata ya Bukuba wilayani hapo na kufanya usafi katika soko wilayani Hapo
Wakati akiwa katika zoezi la upandaji miti Mhe. Mkuu wa wilaya alisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuiongezea kipato shule hiyo lakini kuonesha mfano na somo kwa wanafunzi lakini pia kulinda mazingira na uoto wa asili kwa kuwa miche hiyo hukua kama miti na kufanya mazingira kuwa mazuri na kuzuia au kupunguza mabadiliko ya Tabia ya nchi. Jumla ya miche 800 ya chikichi ilipandwa eneo hilo.
Katika zoezi la usafi pamoja na mambo mengine Mhe. Mkuu wa wilaya amesisitiza uhumuhimu wa kujikinga dhidi ya UVIKO-19 kwa kufuata kanuni za afya kukabiliana na maambukizi lakini pia Kupata chanjo ambayo ni Bure.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi-CCM, watumishi kutokataasisi mabali mbali za umma na wananchi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz