Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Mh Michael Ngayalina amewapongeza Watumishi wastaafu kwa kufanya kazi kwa weledi kwa kipindi chote cha utumishi wa umma na kuwasihi Watumishi wa ajira mpya Wilayani hapa kuiga mfano mzuri wa watumishi hao.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi hao katika hafla iliyoandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ya kuwaaga watumishi wastaafu na kuwakaribisha Watumishi wapya.
Aidha ameongezea kwa kuwasihi kufanya kazi ya kuwatumikia Wananchi kwa weledi bila kuzingatia wapo katika mazingira ya ugenini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Mh Isaac Mwakisu ambae aliongozana na wageni mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh Dkt Rashid Chuachua,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ndug Chiriku Chilumba,Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kasulu mji Ndug Vumilia Simbeye amewapongeza watumishi hao na kuwasihi kudumisha umoja na upendo ambao unatengenezwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Mkurugenzi wake.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh Dkt Rashid Chuachua amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi kwa uongozi wake wenye kujali watumishi wake kwa kuwaweka pamoja ili kudumisha umoja wao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz