Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mhe. Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameikabidhi gari hiyo mapema leo katika hafla fupi iliyofanyika Ofisi za Elimu wilayani hapa.
Mhe. Gaguti alitumia fursa hiyo kuwaasa wataalamu wa idara ya Elimu kwamba lazima wahakikishe chombo hiki kinatumika kwa matumizi sahihi ikiwemo kuchangia kuongezeka kwa ufaulu wa Wanafunzi kwa Shule za Msingi na Sekondari.
“Chombo hiki kiwe chachu ya kuongeza ufaulu wa Wanafunzi kwa kusafirisha Walimu na Wataalamu ili kutoa elimu kwa jamii hasa zile zilizokuwa hazifikiki kwa upungufu wa vyombo vya usafiri.”-Gaguti.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Anosta Lazaro Nyamoga ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa msaada huo na kuwasisitiza wataalamu wake kuchapa kazi zaidi ili kuongeza ufanisi hasa katika nyanja ya Elimu na kwamba siku moja Buhigwe ishike nafasi ya kwanza kwa ufaulu kitaifa.
Aidha Afisa Elimu Msingi Ndg. Fred Fandey na Afisa Elimu Sekondary Madam Mbehoma wameupokea msaada huo kwa moyo wa shukrani huku wakiihakikishia serikali kwamba gari hilo litatumika kwa kazi iliyopangwa na si vinginevyo.
“Tunaishukuru Serikali ya Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kwa kusikia kilio chetu cha muda mrefu.” Walimalizia Maafisa hao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz