Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka watumishi wa Umma wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kujituma na kushirikiana miongoni mwao ili kuleta matokeo chanya yatakayoacha alama katika Jamii.
Andengenye ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe aliposhiriki hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi hodari kwa Mwaka 2023/2024 waliotambuliwa na Halmashauri hiyo kupitia maadhimisho ya Mei Mosi 2024, na kuwasisitiza kujituma ili kuyafikia malengo yaliyowekwa.
Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mhe Col Michael Masala Ngayalina amewakumbusha watumishi hao kudumisha maadili ya utumishi wa Umma sambamba na kuheshimu utumishi wao.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndug George Mbilinyi amesema utoaji wa motisha kwa watumishi wa Umma daima huleta chachu katika utafutaji na upatikanaji wa matokeo chanya.
Hafla hiyo iliyofanyika Mei 4, 2024 imehudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Deogratias Sangu, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu, Katibu Tawala wilaya ya Buhigwe, Kamati ya Usalama Mkoa na Wilaya ,Viongozi wa dini na siasa, wakuu wa Taasisi , wakuu Idara na Vitengo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz