Mkutano maalamu wa Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali za mwaka wa fedha 2022/2023 uliofanyika leo Tarehe 20 Juni 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Aidha Mh. THOBIAS ANDENGENYE Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kutekeleza hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia ukaguzi wa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa kutekeleza na kufunga hoja 24 kati ya 39.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe: Venance Kigwinya Mwenyekiti wa baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe ameshukuru Uongozi wa Mkoa, Mkaguzi Mkuu wa nje, Baraza la madiwani na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri kwa ushirikiano walioonesha katika kutekeleza mapendekezo na kupelekea kufunga hoja 24 kati ya 39 zilizojitokeza mara baada ya taarifa ya mwaka wa fedha 2022/2023 kutolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz