Wakazi Wilayani buhigwe wametakiwa kujenga tabia ya kutunza maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kupanda miti rafiki kwa mazingira ili kutoathiri vyanzo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Leo mei 29,2024 alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya Munanila nyakimue mulera Biharu iliyopo Wilayani buhigwe na kusikiliza kuwa suala la kuchangia gharama za uendeshaji wa huduma za upatikanaji wa maji ni muhimu ili kufanya kuwa endelevu.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa RUWASA wilaya ya Buhigwe Ndg Golden katoto amesema kuwa mradi wa maji wa Munanila -Nyakimue unatekelezwa kwa thamani ya shiling Billion 9.7 fedha kutoka serikali kuu ambapo utakapokamilika utahudumia wakazi 66,405 katika vijiji 8 vya bweranka kibande kitambuka nyakimue mkatanga kibwigwa Munanila na msagara Wilayani Buhigwe.
Sambamba na utekelezaji wa kazi hizo mh katoto amesema kazi zingine zinazotarajiwa kufanyika ni ujenzi wa matanki mawili ya kuhifadhia maji yatakaoyokuwa na ujazo walita 1,000,000 Kila moja katika Kijiji Cha bweranka na mkatanga.
Aidha ameyataja matarajio ya RUWASA Wilayani Buhigwe kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 72.2 Hadi 90.2%.
Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa Mkoa Pia amepata wasaa wa kutembelea chanzo Cha maji kilichotengenezwa na walengwa wa Tasaf katika Kata ya Biharu na kuongea na wananchi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz