Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina leo tarehe 10 mwezi Juni 2025 amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa bila malipo katika Wilaya ya Buhigwe
Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika kijiji cha Munyegera kata ya Munyegera amesihi Wananchi wote kutumia vyandarua hivyo kwa lengo lililokusudiwa.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassani anatupenda na kutujali na ndo mana akatuletea vyandarua vilivyotiwa dawa hivyo niwasihi Wananchi wenzangu tukatumie vyandarua hivi kwa lengo lililokusudiwa la kumaliza tatizo la maambukizi ya ugonjwa wa Malaria,na kwa namna ya pekee tunamshukuru Rais wetu kwa kuangazia sekta ya Afya na kuiimarisha zaidi”Amesema Kanali Michael Ngayalina
Katibu Tawala Wilaya ya Buhigwe Utefta Mahega amewaasa wakina mama hasa Wajawazito kuhakikisha kila siku wanalala katika vyandarua vyenye dawa ili kumaliza tatizo la ugonjwa wa Maralia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya sita inawapenda na kuwajali Wananchi wake na ndo mana inahakikisha inatatua changamoto zinazowakumba Wananchi ikiwemo wa Munyegera kwa kuwaletea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Shule na Zahanati.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Dkt Innocent Mhagama amesema jumla ya Kaya 51,828 zinatarajiwa kunufaika na mpango wa ugawaji wa vyandarua 168,353 vilivyotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ikiwa ni utekelezaji Mpango wa Taifa wa kudhibiti Maralia(NMCP).
Kwa upande wao wananchi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya hiyo Tito Fumawicha wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwaletea vyandarua vitakavyowasaidia kujikinga dhidi ya mbu waenezao ugonjwa wa maralia sambamba na kuwataka wananchi wenzao kutumia vyandarua wanavyogawiwa kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz