Kama wadau wa lishe katika Wilaya yetu ya Buhigwe tunapaswa kuwajibika kila mmoja kwa eneo lake kuhakikisha udumavu kwa watoto unatoweka kwa kuhakikisha lishe bora inatolewa kwa kuzingatia makundi makuu matano ya vyakula yaani wanga, protini, vitamini, mafuta na madini ambavyo vinapatikana katika maeneo yetu kwa gharama ndogo. Hayo yalisemwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col. Michael M. Ngayalina wakati akifungua kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa ofis ya Mkurugenzi Mtendaji Buhigwe eneo la Bwega hivi karibuni.
Kwa upande wake Afisa lishe wilaya; Madam Theodora Thomas alieleza makundi makuu matano ya vyakula ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika lishe hasa kwa watoto.
Virutubishi: Wanga
2.Vyakula vya aina ya mikunde na vyenye asili ya wanyama
Virutubishi: Protini
3.Mboga-mboga
4.Matunda
5.Mafuta na Sukari
virutubishi: mafuta
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz