Mtendaji wa Kijiji Cha Kasumo amwalika Mkuu wa wilaya ya Buhigwe mh. Col Michael Masala Ngayalina Mei 31,2024 kukabidhi madawati 100 yenye thamani ya shiling million tatu,3000,000 fedha za mapato ya ndani ya kijiji Cha Kasumo.
Ngayalina amekabidhi madawati hayo kwa uongozi wa shule za msingi Kasumo na Lemba ambazo zinaptikana katika Kata ya Kajana.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Ndg George Emanuel Mbilinyi amempongeza mtendaji wa Kijiji Cha Kasumo Bi Angela L. Steven kwa ubunifu huo na usimamizi mzuri wa matumizi ya rasilimali fedha na kuwataka wengine kuiga mfano huo ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbali mbali katika Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz