Katika kuboresha huduma za kisheria nchini bodi ya kitaifa ya Msaada wa Kisheria imetoa wito kwa wadau wa kisheria Wilayani Buhigwe Mkoa wa Kigoma kuwasadia wananchi kutambua haki zao za msingi.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Saulo Malauri ametoa wito huo leo tarehe 23 Sepatemba 2025 walipo tembelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ili kutathimini utoaji wa huduma hizo kwa wananchi kwa wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo wajumbe wa bodi pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi wa huduma za Msaada wa Kisheria Ester Msambazi wamezungumza na wadau mbalimbali wa huduma za kisheria ikiwemo Buhigwe Paralegal Organization (BUPAO) na kuwaasa kuhakikisha wanatoa Elimu ya sheria kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Christopher Kajange akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisheria.
Kajange ameongeza kuwa watumishi wanaohudumia dawati la sheria ambao walipelekwa wilayani humo na Wizara ya Katiba na Sheria wameleta mabadiriko makubwa katika masuala ya sheria.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz