Akizungumza na kujibu maswali yenye utata juu ya chanjo ya Ugonjwa wa UVIKO-19, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewataka wazee kujitokeza kupata chanjo hiyo ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo lakini pia kupunguza maambukizi. Akiwa katika moja ya ziara zake kukagua miradi itakayotembelewa na Mwenge mkuu huyo wa wilaya alikutana na hadhira hiyo ya wazee waliofika kwenye shule ya msingi Nyamasovu, Munanila Buhigwe kwa ajili ya vitambulisho vyao vya wazee ndipo alipoata wasaa kutoa elimu hiyo na mara moja Wataalamu walifika kutoa huduma hioyo ya uchanjaji
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz