Mkuu wa Mkoa wa Kigoma mh Thobias Andengenye Leo February 13,2024 amefungua na kuongoza kikao kazi Cha timu za menejimenti nane za Halmashauri za mkoa wa kigoma kinachofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji kasulu
Kikao hicho kimelenga kukutanisha wakurugenzi na wataalamu kutoka maeneo yote ya Mkoa huo ili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja kuelekea utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ufanisi ikiwa yenye kujibu kero na kutatua changamoto za wananchi.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa amesisitiza swala la mawasiliano na uhusiano mzuri juu ya viongozi na timu za menejimenti ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufasaha na kwa Ushirikiano wa kutosha asiwepo mtu yeyote wa kuogopa mwenzake Wala aliye juu yake make wote tuko sawa!.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz